Matukio

Wasifu

Mhandisi Ronald M. Lwakatare

Mhandisi Ronald M. Lwakatare

Mtendaji Mkuu

Mhandisi Ronald Muberwa Lwakatare ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Mhandisi Lwakatare ana elimu ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Uhandisi wa Ujenzi, na Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Ujenzi wa Barabara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ni mtumishi wa umma kwa miaka kwa 25.

Mhandisi Lwakatare alianza kazi 1993 katika Wizara ya Ujenzi akishika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Naibu Meneja wa Mfuko wa Barabara. Mnamo Januari 2016 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka ambayo iko chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mojawapo ya majukumu makubwa ya Mhandisi Lwakatare katika Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ni kusimamia mradi wa DART. Mradi wa DART unatekelezwa katika awamu sita zenye urefu wa kilomita 141. Awamu ya kwanza ambao ilianza kutekelezwa mnamo Mei 2016 ina urefu wa kilomita 20.9. Mradi wa DART unaendeshwa katika ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi.