Awamu ya pili ya mradi inajumuisha barabara za Kilwa (kutoka katikati ya Jiji hadi eneo la Mbagala Rangitatu), Sokoine Avenue (kutoka mtaa wa Zanaki hadi mzunguko wa Gerezani), mtaa wa Gerezani (kutoka mzunguko wa Gerezani hadi Kamata kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Msimbazi), mtaa wa Bandari (kutoka mzunguko wa Gerezani hadi Bendera tatu), barabara ya Chang'ombe (kutoka mzunguko wa Jitegemee hadi VETA kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Kawawa) na barabara ya Kawawa Kusini (kutoka VETA kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Chang'ombe hadi Magomeni kwenye makutano ya barabara za Kawawa na Morogoro) ikiwa na jumla ya kilomita 20.3.
Ujenzi wa barabara katika Awamu hii ulianza rasmi mwezi Mei, 2019 ambapo hadi sasa ujenzi umekamilika na huduma inatolewa.