Mha. Fanuel Kalugendo
Mkurugenzi wa Maendeleo ya usafirishaji
Wasifu
Mha. Fanuel O.S. Kalugendo ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Sifa
Mha. Kalugendo ni Mhandisi wa Mtaalam wa Ujenzi aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania. Mha. Kalugendo ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Uhandisi wa Ujenzi aliyebobea katika Mipango na Usafiri kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Delft kilichopo nchini Uholanzi. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Usimamizi wa Maafa kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Tanzania. Vilevile Mha. Kalugendo ana Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania.
Uzoefu wa Kazi
Mha. Kalugendo ni mtaalamu wa mipango ya Usafiri, na Usimamizi wa Maafa mwenye uzoefu wa kazi katika miradi ya uhandisi, programu ya usimamizi wa majanga na maafa katika sekta ya umma na binafsi. Amejipambanua kitaaluma katika nyanja za: usafiri na usafirishaji wa kitaifa na kimataifa; ushirikiano wa umma na binafsi; program ya kupunguza athari za maafa; pamoja na majadiliano na usimamizi wa mikataba. Pia ana uzoefu wa usimamizi wa miradi mikubwa ya ujenzi na uzoefu katika programu mbalimbali za menejimenti ya maafa kwa zaidi ya miaka 17. Pia ni mshauri wa masuala ya sera, na mikakati ya uendeshaji katika sekta ya usafirishaji.