YAH: KADI YA MWENDOKASI KWA SHILINGI 1,000/- TU!
YAH: KADI YA MWENDOKASI KWA SHILINGI 1,000/- TU!
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) unautaarifu umma kuwa ili kusafiri kwenye mfumo wa DART, kila msafiri anapaswa kuwa na Kadi ya Mwendokasi. Katika kuboresha huduma na mfumo wa ukusanyaji wa nauli pamoja na kuruhusu wateja wetu kutumia kadi, bei ya kadi hii imeshushwa hadi Sh 1,000/= (Yaani Shilingi Elfu Moja tu) kuanzia tarehe 17 Mei, 2025.
Matumizi ya tiketi za karatasi yatafutwa rasmi ifikapo tarehe 30 Juni, 2025. Baada ya tarehe hiyo, wasafiri wenye kadi pekee ndio watakaoweza kusafiri kwa kutumia mabasi ya mfumo wa DART. Utaratibu wa matumizi ya kadi hautahusisha wanafunzi.
NUNUA KADI YA MWENDOKASI LEO, SAFIRI KWA HARAKA NA UHAKIKA!
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka – DART
Tarehe: 16 Mei, 2025