Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Wanachama wa DART-SACCOS wafanya uchaguzi wa viongozi
28 Jun, 2023
Wanachama wa DART-SACCOS wafanya uchaguzi wa viongozi

Watumishi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART) ambao pia ni wanachama moja kwa moja wa Chama cha Akiba na Mikopo cha DART (DART SACCOS) Juni 21,2023 wamefanya uchaguzi wa kwanza wa kuchagua Viongozi wa wakukiongoza chama hicho.

 

Uchaguzi huo uliofanyika katika Ofisi za Wakala zilizoko Ubungo Maji Dar es salaam umehusisha chaguzi za viongozi wa nafasi zifuatazo Wajumbe saba wa Bodi, Kamati ya Usimamizi nafasi tatu, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.

 

Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa ni Bibi. Amina Masimba, Bi. Halima Kandoro, Wakili Chevawe Mberesero, Bibi. Caroline Maeda, Bw. Christopher Mabada, Bw. Silla Okumu na CPA. Ramadhan Kihadala.

 

Aidha, Wanachama waliochaguliwa kuwa katika Kamati ya Usimamizi ni Bw. Muston Mwakyoma, CPA. Emanuel Blaxton na CPA. Ezekiel Nyaisara

 

Hata hivyo kwakua kanuni za chama hicho zilielekeza Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti kuchaguliwa miongoni mwa Wajumbe wa Bodi, wanachama hao wa DART SACCOS walimchagua Wakili Chevawe Mberesero kuwa Mwenyekiti na Ndugu Christopher Mabada kuwa Makamu Mwenyekiti.

 

 

Akiongea baada kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Wakili Chevawe alimshukuru Mtendaji Mkuu wa DART ambaye ndiye pia mlezi wa chama hicho kwa kumwamini na kumteua katika kamati ya mpito iliyokuwa na lengo la kufanikisha uanzishwaji wa DART SACCOS.

 

“Awali ya yote napenda kumshuru Mwenyezimungu kwa kutujalia uhai sisi sote tulioko hapa. Pili nimshukuru Mtendaji Mkuu wetu Dkt. Mhede kwa kuniamini na kuniteua kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya mpito katika kufanisha hili. Nafurahi kwamba nafasi ile niliitumia vyema kwa kujituma kwa moyo wangu wote na nashukuru leo limetimia” alisema Wakili Chevawe. “Niwashukuru pia wanachama wenzangu kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi, nawaahidi mambo mazuri yanakuja.”

 

Awali akizungumza na Wanachama, Mlezi wa Chama hicho Dkt. Edwin Mhede alitoa rai kwa wanachama kujitoa kwa kuweka akiba ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujipatia maendeleo yenye faida kwa familia zao na taifa kwa ujumla.

 

 

Mpaka kufikia Juni 21, 2023, Wanachama 86 walikuwa wamesajiliwa kujiunga na kufaidika na DART SACCOSS huku chama hicho kikitegemea kuongezeka kwa wanachama wengine kwani kinapokea yeyote hata kama sio mtumishi wa DART.