Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Anitha Gasper Joseph photo
Wakili Anitha Gasper Joseph

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria

Wasifu

Wakili Anitha Gaspar Joseph ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria DART mwenye mamlaka ya kuhakikisha majukumu yote ya Wakala yanatekelezwa kwa mujibu wa Sheria, hii ni pamoja na utekelezaji wa Amri iliyoanzisha Wakala, usimamizi wa mikataba baina ya Wakala na Watoa Huduma, kutoa ushauri wa kisheria na kuiwakilisha Wakala katika Mahakama au vyombo vingine katika mashauri mbalimbali.

Wakili Anitha ana Shahada ya Sheria LL.B (Degree Bachelor of Laws)na Shahada ya Uzamili LL.M (Master of Laws in Corporate and Commercial Laws) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Cheti cha Kuhitimu Shule ya Sheria ( Law School of Tanzania).

Wakili Anitha ana uzoefu wa zaidi ya miaka 14 katika fani ya Sheria akihudumu katika nafasi mbalimbali kama vile Wakili wa Serikali, Hakimu Mkazi na Msaidizi wa Jaji Mahakama ya Rufani.