Matukio

Kituo cha Mawasiliano

KITUO CHA USIMAMIZI WA HALI YA NYENDO ZA USAFIRI

Mtoa Huduma wa Mpito (ISP) amefunga vifaa vichache vya mfumo wa ukusanyaji nauli kimtandao (AFCS) na mpaka sasa ni juhudi chache zimefanywa kutoa mfumo wa usafirishaji kwaajili ya kufuatilia na usalama wa Mabasi Yaendayo Haraka na watumiaji. Wakala inakusudia kuboresha usalama wa shughuli za mabasi na kuimarisha ufuatiliaji wa usafiri na ukusanyaji wa nauli kwa kuanzisha mfumo kamili wa ITS/AFCS katika awamu yote ya kwanzaya Mabasi Yaendayo Haraka.

Mradi huu utasaidia (i) ufungaji wa vifaa vya ITS na AFCS kwenye njia yote ya DART yenye urefu wa kilometa 21, (ii) ufungaji wa kituo cha usimamizi wa hali na nyendo za usafiri, (iii) kuwajengea uwezo watumishi wa DART, (iv) utafiti kabambe wa mahitaji ya awamu ya 2,3 ya 4 na, (v) uimarishaji wa ITS kwenye laini zote za BRT.