Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Sisi ni Nani?

Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake. Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa jiji la Dar es Salaam. Wakala inakusudia kufikia malengo yafuatayo:

a)Kuanzisha na kuendesha mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka kwaaajili ya Dar es Salaam, yatakayotumia jina la DART;

b)Kuhakikisha mtiririkobora wa usafiri kwenye mitaa na barabaraza mjini, na

c)Kuhakikisha usimamizi wa wakala wenye ufanisi.