Frequently Asked Questions

Kadi zinazotumika sasa hivi ambazo ni laki 2 alinunua mtoa huduma ambaye ni UDART. Kazi hizo baada ya kununuliwa na abiria ni chache zipatazo asilimia 30 zinaonekana katika mfumo na nyingine hazijulikani zilipo. Kutokana na hilo Wakala uliona ni vyema kutokuongeza kadi nyingine mpaka mkusanyaji nauli (fare collector) atakapopatikana ataongeza kadi nyingine na atakuwa na jukumu zima la kusimamia usalama wa kadi. Mchakato wa kumpata mkusanyaji nauli umeanza na kwa sasa umefikia hatua ya majadiliano ya kumpata mkusanyaji huyo mpya. Kadi zitaanza kutolewa baada ya kumpata mkusanya nauli.

Kwanza hii ni huduma ya mpito ambapo ilikuwa itekelezwe kwa muda wa miaka miwili; katika kipindi hicho mtoa huduma alipewa nafasi ya kuingiza mabasi 140. Mabasi hayo yamegawanywa katika njia saba kwenye njia kuu na njia mbili kwenye njia za mlishi. Ili kutoa huduma kamili mpango ulikuwa mabasi yaletwe 305 kwa ajili ya kutoa huduma katika njia saba za njia kuu na njia mbili. Kufikia lengo hilo, Wakala upo katika mchakato wa kumpata mtoa huduma wa pili. Wakala hauwezi kuruhusu matumizi ya daladala kuingia kwenye mfumo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mfumo wetu unaitwa Mass Transit unaotumia mabasi makubwa yenye ujazo maalum (specification) ambao kwa uchache basi moja linabeba abiria hadi 140, wakati daladala hubeba wachache asilimia 25. Pia vituo vyetu vya mfumo vimewekwa tofauti kiasi kwamba abiria hupanda mabasi upande wa kulia na hata eneo la kupandia lipo katika kimo cha mita 0.9 wakati daladala milango yake ipo kushoto na kimo cha mlango hukaribia futi 1. Pia utaratibu wa ukusanyaji mapato wa BRT ni tofauti kabisa na ule wa daladala ambapo kuna mgawanyo kati ya mtoa huduma, wakala na Msimamizi wa fedha (Fund Manager), utaratibu ambao haupo kwenye daladala. Vilevile mfumo unaendeshwa kwa ratiba maalumu kiasi kitakachosababisha kuvuruga ratiba hiyo ili daladala ziingie suala ambalo ni gumu. Kumbuka kwamba kifupi lengo la kuanzisha mradi huu ilikuwa ni kuboresha usafiri wakazi wa jijini Dar es salaam na kuondoa mlundikano wa mabasi katikati ya mji kwa kuleta mabasi makubwa na kisasa yatakayotumia muda mfupi kwa usafiri, Hivyo tunawasihi wananchi kuwa wavumulivu katika kipindi hiki ambapo anasubiriwa mtoa huduma wa mabasi ndipo mabasi mengine yaweze kuongezwa.
Kwa utaratibu wa kawaida, mtoa huduma huweka mabasi barabarani asilimia 100 ya mabasi wakati abiria wakiwa wengi (peak hr) na mabasi asilimia 75 -84 wakati abiria wakiwa wachahche (off peak). Hapo awali, kabla ya Karakana ya Jangwani kukumbwa na mafuriko mabasi yalikuwa yanaenda kuegeshwa kwenye Karakana ya Jangwani, pindi inapotoka (peak hour) kwenda (off peak). Ila kipindi ambacho mafuriko yalitokea mabasi yalikuwa yanaegeshwa maeneo tofauti hasa katika vituo vikubwa. Pia madereva huwa wanaegesha mabasi kwa kuzingatia ratiba maalum ya mabasi ambayo imeandaliwa na wataalam kwa kuzingatia mahitaji ya usafiri katika njia husika.
Tarehe 05/05/2017 Wakala ulitoa tangazo kuhusu kupatikana kwa mtoa huduma ambapo mchakato huo haukufikia mwisho kwa sababu PPRA (Public Procurement Regulatory Authority) alishauri mchakato uanze upya ili kutoa nafasi sawa kwa wazabuni kwa sababu mmoja wa wazabuni alilalamika kutokupewa majibu ya maswali aliyoulizwa kwa wakati. Hivyo, mchakato ulirudiwa tena ambapo tarehe 16/08/2017 wazabuni walipewa nyaraka za zabuni na baada ya wazabuni kurejesha nyaraka hizo tarehe 05/09/2017 ufunguzi ulifanyika mpaka uchambuzi wa zabuni ulikamilika. Tarehe 20/03/2018 barua ya tuzo ya zabuni (Letter of Award) ilitolewa na tarehe 29/03/2017 majadiliano kati ya Wakala na mshindi yalifanyika, lakini mtoa huduma ya mpito (U|DART) alisababisha majadiliano kusitishwa aliishtaki Wakala mahakamani tarehe 2702/2018 hukumu ilitoka na Wakala ilishinda hiyo kesi. Hata hivyo, hakuridhika na hiyo hukumu na tarehe 10/04/2018 aliishtaki tena Wakala hivyo kusitisha zoezi zima la majadililiano na mzabuni aliyeshinda. Hukumu hiyo ya kesi itatolewa tarehe 07/02/2018. Hivyo baada ya kumpata mtoa huduma huyo mabasi yataongezwa ili kuboresha usafiri jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa tatizo la uchelewaji wa mabasi katika vituo inatokana na uchache wa mabasi, pia inapotokea mafuriko katika eneo la Jangwani na kusababisha sehemu ya kufanyia huduma mabasi kujaa maji; mtoa huduma anashindwa kufanya huduma kwa wakati hivyo mabasi kuchelewa kwenye vituo. Pia, mtoa huduma kushindwa kufata ratiba ya mabasi iliyowekwa kati yake na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka.
DART imepata hasara mbalimbali ikiwemo abiria wake kukosa huduma kwa wakati kutokana na ubovu wa baadhi ya mabasi hali iliyosababishwa na mafuriko ya mwezi Aprili hadi Mei, pia hasara ya kugharamia urekebishaji wa mabasi yaliyoharibika, kusafisha karakana, mitaro na barabara wakati wa mafuriko. Hasara nyingine ni kushuka kwa mapato ya kila siku kutokana na uchache wa mabasi.
Kwa ushirikiano na TANROADS, Wakala wa DART umekuwa ukiondoa uchafu na mchanga katika mto Msimbazi eneo la Jangwani ili kurahisha upitaji wa maji. Zaidi ya hiyo, kuna mpango wa muda mrefu unaofanywa na Mradi wa DMDP (Dar es Salaam Metropolitan Development Programme) chini ya TAMISEMI na Halmashauri zote za jiji la Dar es Salaam. Mradi huu chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia unaogharamia kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayoikumba bonde la Msimbazi hususan mafuriko. Mpaka sasa wameshamshirikisha mtaalamu ambaye anafanya usanifu wa kitu gani kifanyike ili Jangwani na bonde zima la Msimbazi lisikumbwe na majanga ya mafuriko.

Kwanza mazingira ya awali ya Jangwani hayakuwa kama hali ilivyo sasa kwa sababu eneo hilo lilikuwa na eneo kubwa la kuhifadhi maji, kina cha daraja kilikuwa karibia mita 4 na pia mikoko katika daraja la Salenda ilikuwa michache hivyo kupitaji wa maji kutoka mto Msimbazi kwenda baharini ulikuwa rahisi. Hivyo, kabla ya ujenzi wa karakana katika eneo la Jangwani kulifanyika Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact Assessment) na kubaini kuwa eneno hilo linafaa baada ya tathmini hiyo kueleza namna ya kukabiliana na athari chache zitakazoweza kujitokeza; pia ujenzi wa karakana ulinyanyuliwa mita 2 juu. Hata hivyo siku za karibuni eneo la mto Msimbazi limepoteza uhalisia wake na kusababisha mafuriko na athari nyingine kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu katika maeneno ya juu na ndani ya bonde la Msimbazi kama vile kuanzishwa kwa soko, uwepo wa barabara ya Kigogo kwenda Jangwani, shughuli za kibinadamu zinazoleta udongo, chupa na mifuko ya plastiki kuelekea mto Msimbazi, sababu hizi zimechangia kina cha daraja kupungua kutoka mita 4 hadi chini ya mita 1; kutokana na hali hii, maji kujaa sana katika daraja wakati wa mvua nyingi, pia kuongezeka kwa mikoko katika daraja la Salenda kunazuia upitaji wa maji kutoka bonde la Msimbazi kwenda Baharini.