Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mabasi Mlishi

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) inatoa huduma ya mabasi katika Njia Mlishi tano zilizopo katika Mradi wa DART Awamu ya Kwanza. Njia Mlishi ni zile barabara ambazo hutumiwa na vyombo vyote vya usafiri tofauti na Njia Kuu za Mabasi Yaendayo Haraka ambazo hutumiwa na mabasi hayo pekee. Hivyo lengo la huduma katika Njia Mlishi hizo ni kuwasafirisha abiria mpaka katika Njia Kuu ya Mabasi Yaendayo Haraka ili waweze kusafiri kule waendapo kwa haraka zaidi na kuwarudisha katika maeneo yaliyo nje ya Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Huduma ya Mabasi katika Njia Mlishi za Mradi wa DART Awamu ya Kwanza hutolewa kutokea;

  • Kituo Kiuu cha Kimara hadi Kituo Mlishi cha Mbezi Luis
  • Kituo Kikuu cha Kimara hadi Kituo Mlishi cha Magufuli Terminal
  • Kituo Kikuu cha Kimara hadi Kituo Mlishi cha Kibaha
  • Kituo Kikuu cha Kimara hadi Kituo Mlishi cha Hospitali ya Mloganzila
  • Kituo Kikuu cha Gerezani hadi Kituo Mlishi cha Hospitali ya Muhimbili