Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Ushauri katika BRT

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka umekasimishwa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa Mradi wa DART katika Awamu sita. Mradi wa DART unatekelezwa kwa kuimarisha miundombinu iliyokuwapo, usimamizi wa upatikanaji wa mtoa huduma ya Mabasi, mkusanya nauli pamoja na meneja wa Fedha.

Awamu ya Kwanza ya Mradi wa DART inayopita katika barabara ya Morogoro ikiwa na urefu wa kilomita 20.9  ilianza kutoa huduma mwezi Mei 2016 kupitia Mtoa Huduma ya Mpito. Kuanza kwa huduma katika Awamu ya kwanza ya Mradi wa DART kumevutia makundi mbalimbali kutoka nchi nyingi za Africa kufika nchini kwa lengo la kujifunza ni namna gani Tanzania imeweza kutekeleza mradi wa Mabasi Yaendayo haraka licha ya kuwepo kwa sababu nyingi mtambuka.

Ili kutoa ufafanuzi wa kina wa namna gani mradi unatekelezwa katika jiji la Dar es salaam, Watumishi wa DART wamekuwa wakitoa mafunzo kupitia uwasilishaji mada kwa njia ya Power point  kwa wageni kutoka Taasisi mbalimbali wanaotembelea Mradi wa DART na pande zote kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu. Mbali kuwasilishiwa mada kuhusu Mradi wa DART na utekelezaji wake katika Jiji la Dar es salaam, Wakala pia umekuwa ukiwatembeza wageni hao katika ushoroba wa Mabasi Yaendayo Haraka ili kujionea shughuli za uendeshaji zinavyofanyika.

Baadhi ya nchi zilizotuma Wataalam wake kuja kujifunza kuhusu Mradi wa DART Dar es salaam kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita ni Kenya, Uganda, Ethiopia, Rwanda, Algeria, and Nigeria.