Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Maeneo ya Matangazo

Ushoroba wa Mradi wa  DART  ni sehemu ya kuvutia ambayo kampuni za ndani na za kimataifa zinaweza kutumia kutangaza bidhaa zao kuhusiana na sifa, vifurushi vya bidhaa. Kwa sasa tunazo  kampuni chache za matangazo, Wakala unapenda kuzikaribisha kampuni nyingine kutumia fursa hii kuja  kutangaza katika ushoroba wa Mradi wa DART  ili kuongeza wateja katika biashara zao. Maeneo ya matangazo ni pamoja na Madaraja ya Watembea kwa Miguu, Vituo vidogo na Vituo vikuu, Fursa ya kuvipa vituo majina, kutangaza katika Mabasi pamoja na katika kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Wakala wa DART.