Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Wenye Uhitaji Maalum

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umeendelea kuwajali Abiria wenye Mahitaji Maalum kwa kuwapatia kipaumbele wakati wa kupata huduma katika Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka. Miongoni mwa wanufaika hao ni Wamama Wajawazito, Wazee, Wagonjwa pamoja na Walemavu.

Aidha katika kuwadumia Walemavu wa Viungo, Wakala wa DART unatoa huduma ya Viti mwendo katika Vituo Vikuu vya Mabasi Yaendayo Haraka kwa lengo la kuwarahisishia abiria hao kutoka na kuingia kwa urahisi katika Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka kupitia vivuko vya madaraja ya watembea kwa miguu.