Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Maegesho

Katika ushoroba wa DART baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya huduma za maegesho ambapo abiria  au wahitaji wengine wa huduma ya maegesho wanaweza kuhifadhi vyombo vyao vya usafiri kwa kulipa ada ya maegesho. Miundombinu ya maegesho inatarajiwa kuwepo katika awamu zote za mradi  ili kuwezesha wamiliki wa vyombo binafsi vya usafiri kuegesha vyombo vyao na kuunganisha safari kupitia Mabasi Yaendayo haraka au usafiri mwingine. Kwa hivi sasa kuna maegesho ya muda mfupi katika Kituo cha Gerezani na Kivukoni ambapo Daladala, Pikipiki za miguu mitatu maarufu Bajaji  na magari ya watu binafsi yananufaika kwa kulipa ada ndogo ya maegesho. Kwa awamu ya pili, Wakala wa DART amejenga vituo vya maegesho katika Kituo Kikuu cha Mbagala Rangi tatu na Kituo kidogo cha Mtoni kwa Azizi Ally.