Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mabasi Ya Wanafunzi

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umewapa umuhimu wa pekee kundi la Wanafunzi wanaosoma shule za kando kando ya Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka pale wanapoelekea shule nyakati za asubuhi na vilevile wanaporudi nyumbani nyakati za jioni.

Wakala wa DART umethamini kundi hilo kwa kuwatengea mabasi maalumu mawili makubwa  nyakati za asubuhi na mawili nyakati za jioni  ambayo huwasafirisha wanafunzi pekee wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa chini ya usimamizi wa Maafisa wa Huduma za Jamii wa Wakala wa DART. Mabasi hayo huanzia safari zake katika Kituo Kikuu cha Kimara hadi Gerezani na Kimara hadi Kivukoni nyakati za asubuhi  na kwa wakati wa jioni kuanzia Kituo Kikuu cha Gerezani na Kivukoni hadi Kituo Kikuu cha Kimara. Ratiba za mabasi ya Wanafunzi ni kama zinavyoonekana hapo chini.

 

Na.

KUTOKA

MUDA

KWENDA

1.

KIMARA

12:00 ASUBUHI

GEREZANI

2.

KIMARA

12:20 ASUBUHI

KIVUKONI

3.

KIVUKONI

10:30 JIONI

KIMARA

4.

GEREZANI

11:00 JIONI

KIMARA