Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Kadi ya Mwendokasi
Kadi ya Mwendokasi

Kadi ya Mwendokasi ni nini? 

Hii ni Kadi Janja inayotumika kufanya malipo ya nauli katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka.

                     

                

Inaokoa muda Hakuna haja ya kubeba fedha Hakuna haja ya kubeba fedha Inaepusha kusimama katika foleni ndefu ya kukata tiketi

 

Nawezaje kupata Kadi ya Mwendokasi?

Tembelea Vituo Vikuu na Vituo Vidogo vya Mabasi Yaendayo Haraka.

Ada na Kiwango cha kuweka fedha katika Kadi ya Mwendokasi

  • Kiwango cha juu cha kuweka fedha katika kadi hakipaswi kuzidi shilingi 30,000/=
  • Kiwango cha chini kuweka salio katika kadi ni shilingi  1,000/=

Kadi ya Mwendokasi inagharimu kiasi gani?

Kadi ya Mwendokasi inaweza kupatikana kwa kulipia kiasi cha  /= . Kiasi hiki kinahusisha malipo ya awali.

Ni namna gani naweza kuweka fedha katika Kadi ya Mwendokasi?

Ili kuweka fedha katika kadi tafadhali tembelea Ofisi za Wakala wa DART zilizopo katika Vituo vidogo na Vituo Vikuu vya Mabasi Yaendayo  Haraka.

Kutokana na kukua kwa teknolojia, malipo ya kabla ya nauli ya Mabasi Yaendayo  Haraka kupitia Kadi ya Janja ya Mwendokasi, yanaweza kufanyika kwa miamala ya simu kama vile  M-Pesa, Airtel Money, Tigo-Pesa nakadhalika.

Ili kuweka fedha katika Kadi ya Mwendokasi kupitia simu yako ya mkononi, kwa umakini fuata hatua zilizowekwa na endapo utakuwa na wasiwasi wowote kuhusu hilo, usisite kuwasiliana na Maafisa wa DART walioko katika Vituo Vikuu u Vidogo vya mabasi Yaendayo haraka na maeneo zinakouzwa kadi hizo. 

Kurudisha Kadi yako iliyopea au kuharibika

Endapo Kadi yako Mwendokasi imepotea, imeharibika au haifanyi kazi, unaweza kuomba nyingine kwa kuambatisha nyaraka na taarifa zilizotumika kusajili kadi ya awali. Kiasi cha fedha kilichobaki katika Kadi iliyopotea kitahamishiwa katika kadi yako mpya. 

Utatakiwa kulipia tena ili kurudisha kadi iliyopotea au kuharibika. Baada ya kukamilisha taratibu za kurudisha Kadi yako iliyopotea au kuharibika, utasubiri kwa muda wa siku saba (7) ili kiasi cha fedha kilichokuwapo katika Kadi ya awali kuhamishiwa katika Kadi mpya. Hivyo ili kurudisha Kadi iliyopotea au kuharibika, tafadhali tembelea Kituo Kikuu au Kituo Kidogo cha Mabasi Yaendayo Haraka chochote kilicho karibu au jirani na wewe.

 

Mambo ya muhimu kuhusu Kadi ya Mwendokasi

  • Hutaweza kutumia Kadi hii kununulia biadhaa au huduma kwa njia ya simu au kupitia mtandao.
  • Kila muamala utakaofanyika kupitia Kadi ya Mwendokasi, utakatwa haraka katika salio lililopo.
  • Hata pale Kadi ya Mwendokasi inapotumika pasipo uwepo wa mtandao, salio lililopo katika Kadi litatolewa pasipo kuchelewa sehemu itakapokuwepo kadi hiyo.

Nawezaje kutumia Kadi ya Mwsendokasi?

  1. Gusisha Kadi yako ya Mwendokasi au Tiketi ya Karatasi yenye Msimbokodi katika Geti la kulipia nauli mpaka pale utakapoona mshale wa kijani ukikuruhusu kuendelea.
  2. Pindi uwapo katika Kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka, subiri basi lisimame katika jukwaa la kupandia. 
  3. Pale unapoingia ndani ya basi chukua taadhari ya uwazi uliopo kati ya basi na jukwaa la kituo.
  4. Tafadhali acha viti vyote vilivyotengwa kwaajili ya watu wenye mahaitaji maalumu kama vile walemavu, wajawazito na wazee. 
  5. Weka akilini kuwa Mabasi Yaendayo Haraka yanakuja kituoni kwa kufuata ratiba hivyo hupaswi kugombania.
Adhabu

 

Hakiki tiketi yako kwa usahihi katika Geti kwani utalipa adhabu usipofanya yafuatayo:

- Ukigusisha Kadi yako katika Geti wakati wa kuingia tu lakini hukufanya hivyo wakati wa kutoka.

- Ukigusisha Kadi yako katika Geti wakati wa kutoka lakini hukufanya hivyo wakati wa kuingia.

- Ukikaa ndani ya Mfumo wa DART kwa muda mrefu yaani zaidi ya dakika 90 baada ya kuingia.

Adhabu ni Shilingi 1,000/=