Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Matangazo

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) unatoa fursa kwa Makampuni na Watu binafsi wanaowiwa kutangaza huduma zao kwa wananchi kupitia Miundombinu ya Mradi wa DART hususani katika Vituo Vikuu, Vituo vya kawaida, Madaraja na kwinginepo kunaponekana kunafaa.

Wateja wengi wanaojitangaza kupitia Mfumo wa DART wameweza kunufaika kwa biashara zao kuonekana na kufahamika na wengi kwani Mfumo wa DART unasafirisha abiria zaidi ya laki mbili kila siku ambao huona na kusikia matangazo husika. Vilevile miundombinu ya Madaraja na Vituo katika Mfumo DART vimesanifiwa vizuri na hivyo kuvutia kutazamwa na wasio abiria wanapopita pembezoni mwa Mfumo wa DART.