Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Dira na Dhamira

Dira ya Wakala ya DART

Kuwa na mfumo wa kisasa wa usafiri wa umma wenye gharama nafuu kwa watumiaji na faida kwa waendeshaji unaotumia mabasi makubwa yenye ubora unaokidhi viwango vya kimataifa, yanayohifadhi mazingira, yatakayopita kwenye njia maalum za mabasi na hivyo kupunguza muda wa safari.

Dhamira ya Wakala ya DART

Kutoa mfumo wa usafiri wa umma ulio bora, unaopatikana na wa gharama nafuu na kuboresha usafiri mjini kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao hatimaye:

  • Utawezesha kupunguza umaskini.
  • Kuboresha hali ya maisha.
  • Utaleta ukuaji wa uchumi endelevu na kuwa kama kiongozi wa uwekezaji wa ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi katika sekta ya usafiri jijini.