Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Fanuel Kalugendo photo
Mha. Fanuel Kalugendo

Mkurugenzi wa Maendeleo ya usafirishaji

Wasifu

Mha. Fanuel O.S. Kalugendo ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Sifa
Mha. Kalugendo ni Mhandisi wa Mtaalam wa Ujenzi aliyesajiliwa  na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania. Mha. Kalugendo ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Uhandisi wa Ujenzi aliyebobea katika Mipango na Usafiri kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Delft kilichopo nchini Uholanzi. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Usimamizi wa Maafa kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Tanzania. Vilevile Mha. Kalugendo ana Shahada ya  Sayansi katika Uhandisi wa Ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania.


Uzoefu wa Kazi

Mha. Kalugendo ni mtaalamu wa mipango ya Usafiri, na Usimamizi wa Maafa  mwenye uzoefu wa kazi katika miradi ya uhandisi, programu ya usimamizi wa majanga na maafa katika sekta ya umma na binafsi. Amejipambanua kitaaluma katika nyanja za: usafiri na usafirishaji wa kitaifa na kimataifa; ushirikiano wa umma na binafsi; program ya kupunguza athari za maafa; pamoja na majadiliano na usimamizi wa mikataba.  Pia ana uzoefu wa usimamizi wa miradi mikubwa ya ujenzi  na uzoefu katika programu mbalimbali za  menejimenti ya maafa kwa zaidi ya miaka 17. Pia ni mshauri wa masuala ya sera, na mikakati ya uendeshaji katika sekta ya usafirishaji.