Bw. Shaban Kajiru
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Wasifu
Ndugu Shaban Kajiru ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, mwenye dhamana ya kusimamia na kuendeleza mawasiliano ya kibiashara. Pamoja na majukumu hayo, anaongoza mikakati ya uhusiano na vyombo vya habari, akijikita katika ubunifu na uwekaji mikakati ya utoaji taarifa kupitia machapisho, vyombo vya utangazaji, na mitandao ya kijamii.
Akiwa mtaalamu wa Uhusiano wa Umma, Ndugu Kajiru ana Shahada ya Uzamili ya Sanaa katika Mawasiliano ya Umma na Shahada ya Sanaa katika Mawasiliano ya Umma, zote kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT). Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika sekta ya habari na mawasiliano, akihudumu kwa ufanisi katika taasisi za sekta binafsi na za umma.
