Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mfumo wa DART Awamu ya Kwanza

Awamu ya kwanza ya mradi wa DART imehusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara inayojumuisha Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara mpaka Kivukoni (kilometa 15.8), Barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni mpaka Morocco (kilometa 3.4) na Mtaa wa Msimbazi kuanzia Fire mpaka Kariakoo (kilometa 1.7). Ujenzi mwingine ni pamoja na Vituo vya Basi 27, vituo vikuu 5, madaraja ya wapita kwa miguu 3 yaliyoko Kimara, Ubungo na Morocco, na Karakana moja iliyopo Jangwani; Vituo Mlishi vya Basi 4 na upanuzi wa Daraja la Mto Msimbazi na makalvati makubwa mawili katika bonde la Jangwani.natengenezwa