Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Mfumo wa DART Awamu ya Tatu

Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi wa DART unapita katika maeneo ya Bararaba ya Nyerere kutoka Gongolamboto kwenda Katikati ya Jiji na eneo la Barabara ya Uhuru kutoka Tazara kwenda Kariakoo mpaka Gerezani ambao una jumla ya Kilomita 23.6.


Serikali ya Tanzania imepata fedha kutoka International Development Association (IDA) chini ya Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya utekelezaji Mradi wa Uboreshaji wa Usafiri jijini Dar es Salaam (DUTP) na inakusudia kutumia sehemu ya fedha hizo za mkopo kulipia gharama stahiki chini ya mkataba wa ujenzi wa Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka, ambao ni Awamu ya Tatu ya Mradi wa DART. Hivi sasa Washauri wa Usimamizi, M/s DOHWA Engineering Co. Ltd na UNITEC Civil Consultants Ltd wanahakiki usanifu na kutayarisha zabuni kwa wakandarasi.
arasi.