Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Domina Madeli photo
Domina Madeli

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria

Wasifu

Wakili Domina Damian Madeli ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Sheria wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Wakili Domina ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sheria kutoka Kituo cha Mafunzo ya Sheria cha Tanzania na Ujerumani na amesoma Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Bayreuth Ujerumani. Domina Madeli ni Wakili wa Mahakama Kuu na Kamishna wa Viapo. Yeye ni mwanasheria maarufu katika nyanja mbalimbali zikiwemo Usafiri wa umma, Ushirikiano wa kikanda hususan  Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Uwekezaji, hususani Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), na ardhi. Ni Wakili wa Mahakama Kuu kwa miaka 15 akiiwakilisha Serikali katika Mahakama Kuu bila kupoteza kesi hata moja. Kesi alizozisimamia  ni pamoja na kesi zilizofunguliwa na wanaharakati mashuhuri dhidi ya maamuzi ya Serikali, na kesi zilizowasilishwa Mahakama Kuu dhidi ya Chama Tawala cha siasa.

Mbali ya Taaluma ya Sheria, Wakili Domina Damian Madeli ni maarufu katika Usimamizi wa Taka na mazingira kwa masomo ya ngazi ya cheti aliyosomea Hyogo na Chuo Kikuu cha Fukuoka nchini  Japani. Amefanya tafiti kuhusu Mkataba wa Uanzishwaji wa Ushirikiano wa Africa Mashariki na Usimamizi wa Mazingira (The Efficacy of the EAC Treaty in Environmental Protection), na ana tuzo (award) ya msimamizi wa mazingira iliyotolewa na Taasisi ya Tafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aliandaa Sheria Ndogondogo za Mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Halmashauri ya Jiji la Tanga, na Halmashauri ya Manispaa Kigamboni. Wakili Domina Damian Madeli pia ni maarufu na mtaalam katika sheria za michezo Nchini. Kati ya mwaka 2014 hadi 2014 alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Katika nyakati tofauti, alikuwa Mshauri Mkuu wa Kisheria wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo alifanikiwa kusaidia uhakiki wa Kanuni za TFF. Aidha, Wakili Domina Damian Madeli, amekuwa msimamizi wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, na Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010 kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali ya Ulinzi wa Mtoto, ambapo pia yeye ni mama mzazi wa kijana mwenye ulemavu wa usonji (autism).