Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Ng'wanashigi Gagaga photo
Ng'wanashigi Gagaga

Mkugurenzi wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Wasifu

Ndugu Ng’wanashigi Gagaga ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) anayetoa uongozi wa kimkakati wa TEHAMA katika Mfumo wa DART. Anawajibika kwa mabadiriko ya kidijitali na michakato kazi , kuwianisha na Mpango Mkakati wa Taasisi na TEHAMA ili kufikia malengo na majukumu mahususis ya Wakala kwa kutumia jitihada na mikakati ya menejimenti na usimamizi mahili wa TEHAMA.

Sifa
Ndugu Gagaga ana Shahada ya Uzamili ya Teknolojia ya Habari aliyebobea katika Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Pia ana Shahada ya Uzamili ya Uongozi  wa Biashara akibobea katika Fedha na Benki kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT). Aidha, Ndugu Gagaga ana Shahada ya Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Amesajiliwa na Tume ya TEHAMA  kama Mtaalamu wa TEHAMA  katika Ukaguzi wa Mifumo mwenye namba ya usajiliP0069 – SAT. Amehudhuria mafunzo na kupata uzoefu mbalimbali wa Mifumo ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na usimamizi wa Mifumo nadhifu wa kuongoza magari (ITS), Mifumo wa Ukusanyaji wa Nauli Kielektroniki (AFCS), na usimamizi wa vituo vya Usimamizi wa mienendo ya magari barabarani (TMC).

Uzoefu wa Kazi
Ndugu Gagaga ana uzoefu kwa zaidi ya miaka 20 katika Sekta ya TEHAMA akihudumu katika mashirika ya  umma na binafsi nchini Tanzania. Aidha ndugu Gagaga amehudumu katika nyadhifa tofauti za TEHAMA zikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Mwanza (MWAUWASA), Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kuhudumia  na ametoa huduma kwenye Mamlaka mbalimbali za Serikali za Mitaa. Amesimamia miradi mbalimbali ya TEHAMA na Huduma za Ushauri kama vile maendelezo ya Mfumo wa Ukusanyaji wa Nauli Kielektroniki , Mfumo nadhifu wa kuongozea magari, na ituo vya Usimamizi wa mienendo ya usafiri,  Mradi wa Programu Tumizi ya Mwendokasi, MUSE, DARTMIS, GoT-AFCS na mifumo ya usimamizi wa Fedha Epicor  katika Halmashauri  mbalimbali za mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Arusha na Manyara. Ameshirika kusimika  mifumo mbalimbali katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza GoT-HOMIS, LGRCIS, PlanRep, DROMAS. Ndugu  Gagaga ni Katibu wa  kamati ya usimamizi wa  TEHAMA DART.