Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
KUANZA KUTUMIKA KWA NAULI MPYA, JUMATATU, 16 JANUARI 2023
09 Feb, 2023

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART unapenda kuwaarifu watumiaji wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART, kuwa kuanzia Jumatatu, tarehe 16 Januari 2023, nauli mpya zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini-LATRA zitaanza kutumika.

Mabadiliko ya nauli hizi ni kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini , SURA YA 413 iliyoipa LATRA jukumu la kupanga nauli za vyombo vinavyotoa huduma za usafiri ardhini.

Nauli iliyobadilika ni kwa watu wazima tu wanaosafiri katika Njia Kuu (Trunk Route) na Njia Mlishi (Feeder Route)