Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
TANGAZO LA MNADA WA HADHARA WA MAGARI NA MALI CHAKAVU
09 Feb, 2023

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka DART unapenda kuutangazia Umma kwamba, utauza kwa njia ya mnada wa hadhara magari manne (4) aina ya “Ford” na vifaa chakavu vikiwemo samani za ofisi, vifaa vya TEHAMA na vifaa vingine. Mnada utafanyika mnamo tarehe 7 Januari 2023 kuanzia saa 4:00 asubuhi katika ofisi za Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka zilizopo Ubungo Maji, Barabara ya Morogoro – Dar es Salaam. Mkabala na Ofisi za TANESCO Ubungo. MASHARTI YA MNADA

1. Mali zitauzwa kama zilivyo, mahali zilipo

2. Mnunuzi magari atalazimika kulipa papo hapo amana (deposit) isiyopungua asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani ya mali husika na atatakiwa kukamilisha malipo yote katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili atakosa haki zote za ununuzi wa chombo husika na amana iliyolipwa haitarudishwa. Aidha kwa vifaa vinginevyo mnunuzi atalazimika kulipa papo hapo asilimia mia moja (100%) ya thamani ya chombo husika.

3. Mnunuzi atatatakiwa kubadilisha umiliki wa gari husika ndani ya kipindi cha miezi mitatu (3).

4. Mnunuzi atatakiwa kuondoa/kuchukua chombo alichonunua si chini ya siku saba (7) kuanzia siku ya kukamilisha malipo. Hii ni kwa magari tu. Aidha, kwa vifaa vya ofisi na vifaa vinginevyo, mnunuzi atatakiwa kukamilisha malipo na kuondoa/kuchukua chombo hicho siku ya mnada.

5. Ruhusa ya kuangalia magari na vyombo husika itatolewa kwa siku mbili (2) kabla ya tarehe ya mnada yaani tarehe 5 Januari 2023 na tarehe 6 Januari 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi hadi saa 09:30 alasiri. 6. Mnada utaanza saa 04:00 asubuhi siku ya Jumamosi mnamo tarehe 7 Januari 2023.

7. Vigezo na masharti ya mnada kuzingatiwa.

8. Tangazo la mnada pia linapatikana katika tovuti ya Wakala pamoja na kurasa za mitandao ya jamii (DARTMwendokasi)

MTENDAJI MKUU

WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA

12 DISEMBA 2022