Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
ONYO DHIDI YA UJUMBE WA UONGO KUHUSU AJIRA NA MAFUNZO
04 Jun, 2025

YAH: ONYO DHIDI YA UJUMBE WA UONGO KUHUSU AJIRA NA MAFUNZO

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART unapenda kuuarifu umma kuwa ujumbe unaosambaa kupitia WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii, unaohamasisha watu kutuma namba zao za simu kwa ajili ya kuomba nafasi za ajira au mafunzo mbalimbali, si wa kweli.

Wakala wa DART haujatoa tangazo lolote linalohusiana na ajira au mafunzo kwa njia ya kutuma namba za simu. Hakuna mchakato wa ajira au mpango wa mafunzo unaoendelea kwa sasa kwa njia hiyo.

Tunatoa rai kwa wananchi kuwa waangalifu na kutoshiriki wala kusambaza ujumbe wowote usio rasmi na usiotolewa kupitia njia halali za mawasiliano za Wakala wa DART.

Tangazo lolote rasmi kuhusu ajira au mafunzo kutoka Wakala wa DART litakuwa limetolewa kupitia tovuti rasmi ya wakala, magazeti yaliyosajiliwa na akaunti rasmi za mitandao ya kijamii.

Wakala wa DART hauhusiki kwa namna yoyote na matumizi mabaya ya jina lake na unatoa rai kwa wananchi kuwa makini na vitendo vya udanganyifu.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART

Juni 3, 2025