Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Muda wa huduma kipindi cha Majaribio katika Mradi wa DART Awamu ya Pili
14 Oct, 2025
Muda wa huduma kipindi cha Majaribio katika Mradi wa DART Awamu ya Pili

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umetangaza saa za huduma kwa kipindi cha majaribio cha Awamu ya Pili ya Mradi wa DART, inayohusu njia ya kutoka Gerezani hadi Mbagala.

Huduma za mabasi kwenye njia hiyo sasa zinapatikana kila siku kuanzia Saa 11:00 Alfajiri na zitaendelea hadi Saa 4:00 Usiku.

Mabadiliko haya ya muda yanalenga kuendelea kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam hususani wanaoishi kando kando ya Barabara ya Kilwa na kupima ufanisi wa huduma kabla ya kuanza rasmi kwa huduma kamili. 

Aidha, abiria wanaetakiwa kuzingatia saa hizi mpya wanapotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika njia ya Gerezani na Mbagala.