News

TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WATAALAM DUNIANI KATIKA MASUALA YA USAFIRI ENDELEVU DUNIANI.


Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano na adha ya usafiri jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam Paul Makonda wakati akifungua mkutano mkubwa wa watalaam wa masuala ua usafiri kutoka katika nchi mbalimbali duniani ambapo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kupitia Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART).

“Kwa muda mrefu jiji la Dar es Salaam limekuwa na msongamano mkubwa wa watu na shida ya usafiri na hivyo kusabababisha adha ya usafiri lakini mara baada ya kuanzishwa kwa Mabasi Yaendayo Haraka tatizo hili limepungua kwa vile ni mabasi yanayotumia muda mfupi kufika.”Alisema Mkuu wa Mkoa.

Aliwaeleza wataalam hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejidhatiti kwa kiasi kikubwa kuendelea kuboresha sekta ya usafiri ili wananchi waweze kusafiri kwa haraka na kupunguza msongamano nchini Tanzania.

Aidha Makonda amesema idadi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam imekuwa ikiongezeka kila kukicha hivyo uwepo wa miundombinu bora ya usafiri itasaidia kupunguza msongamano wa magari unaopelekea serikali kupoteza mabilioni ya fedha kutokana na foleni.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amefungua mkutano mkubwa wa siku tatu wa wataalamu wa masuala ya usafiri kutoka majiji 49 na nchi zaidi ya 30 Duniani waliokuja nchini kujifunza namna Dar es salaam ilivyofanikiwa kwenye usafiri wa mabasi ya mwendokasi na kushika nafasi ya kwanza katika majiji ya Afrika.

Kwa upande wa wataalam hao wamefurahi kuona namna Serikali ilivyojidhatiti kuendelea kuboresha sekta ya usafiri ambapo wameshangaa kuona mipango ya serikali kuendelea kujenga miundombinu ya mabasi mwendokasi hadi awamu ya sita.

Mkutano Mkubwa Kama huu kufanyika Dar es salaam ni heshima kubwa kwa Taifa ambapo wataalamu hao watafanya ziara ya kutembelea miundombinu ya usafiri kwa jiji la Dar es salaam kisha kutoa ushauri na mapendekezo kwa mkuu wa mkoa kwaajili ya maboresho.

Mradi wa abasi yaendayo Haraka unatekelezwa katika awamu sita ambapo ujenzi wa miundombinu katika awamu ya Pili ya Mradi katika Barabara ya Kilwa inatarajia kuanza mapema mwaka huu.Hii ni Tuzo ya pili kupokelewa na Wakala wa Mabasi yendayo haraka ambapo hivi karibuni Taasisi ya C40 ya Marekani iliipa Jiji la Dar es salaam Tuzo ya Usafirishaji endelevu pamoja na Jiji la NewYork la Marekani.

Tanzania Census 2022