Matukio

Iliyokamilika

MFUMO WA DART AWAMU YA KWANZA

Utekelezaji wa awamu ya kwanza wa mradi wa DART ulianza mwaka 2007 nakukamilika mwaka 2015. Awamu ya kwanza ya njia ya DART imehusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara inayojumuisha Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara mpaka Kivukoni (kilometa 15.8), Barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni mpaka Morocco (kilometa 3.4) na Mtaa wa Msimbazi kuanzia Fire mpaka Kariakoo (kilometa 1.7). Ujenzi mwingine ni pamoja na Vituo vya Basi 27, vituo vikuu 5, madaraja ya wapita kwa miguu 3 yaliyoko Kimara, Ubungo na Morocco, na Karakana moja iliyopo Jangwani; Vituo Mlishi vya Basi 4 na upanuzi wa Daraja la Mto Msimbazi na makalvati makubwa mawili katika bonde la Jangwani.