Matukio

MIRADI YA MIPYA YA MABASI YAENDAYO HARAKA

Utekelezaji wa miradi ya DART awamu ya nne, tano na sita.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) kugharimia Mradi wa Kuboresha Usafiri Jijini Dar es Salaam (DUTP) na kukusudia kutumia sehemu ya fedha za mkopo kwa kulipia malipo yanayostahili chini ya mkataba kwaajili ya Usanifu Ujenzi wa awamu ya tano, sita na Ujenzi wa Mfumo ya DART awamu ya nne.