Matukio

Miradi ya DART inayoendelea

UTEKELEZAJI WA AWAMU YA PILI YA MRADI WA DART.

Tarehe 30 Septemba, 2015 Africa Development Bank iliidhinsha mkopo wa kusaidia juhudi za serikali ya Tanzania kupunguza msongamano wa usafiri jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 23 Oktoba, 2015 serikali ya Tanzania imetiliana saini na benki hiyo kugharimia mradi.

Hivi sasa Washauri wa Usimamizi wapo kwenye eneo la mradi ambao ni M/s BOTEK Bosphorus Technical Consulting Corporation ya Turkey kwa kushirikiana na Apex Engineering Co. Ltd ya Tanzania kwaajili ya ujenzi wa barabara na Interconsult Tanzania Limited kwaajili ya majengo.

Mchakato wa kuwapata wakandarasi kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya awamu ya pili ya DARTunaendelea na zabuni ya ujenzi wa barabara imetangazwa mwezi Mei 2018 na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ni tarehe 2 Julai, 2018 wakati tathmini ya zabuni kwaajili ya majengo inaendelea.

UTEKELEZAJI WA AWAMU YA TATU YA MRADI WA DART

Serikali ya Tanzania imepata fedha kutoka International Development Association (IDA) chini ya Benki ya Dunia (WB) kwaajili ya utekelezaji Mradi wa Uboreshaji wa Usafiri jijini Dar es Salaam (DUTP) na inakusudia kutumia sehemu ya fedha hizo za mkopo kulipia gharama stahili chini ya mkataba wa ujenzi wa mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka, ambao ni Awamu ya Tatu ya Mradi wa DART.

hivi sasa washauri wa usimamizi, M/s DOHWA Engineering Co. Ltd na UNITEC Civil Consultants Ltd wanaakiki usanifu na kutayarisha zabuni kwa wakandarasi.

UTEKELEZAJI WA MIUNDOMINU YA MAHALI PAKUEGESHA NA PAKUPANDIA KIMARA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imetenga fedha za Mradi wa Maendeleo katika bajeti ya MTEF mwaka wa fedha 2017/18 na 2018/19 kuwezesha usanifu na ujenzi kwaajili ya ujenzi wa mahali pakuegesha na kupandia na vituo vya basi Kimara Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo unashughulikia shauku ya muda mrefu ya kuboresha upatikanaji na uhamishaji wa huduma za Mabasi ya DART katika kituo kikuu cha Kimara.

Pia ni muhimu kuzingatia kuwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa miundombinu ya mfumo wa DART na shughuli za uendeshaji mabasi tarehe 25 Januari, 2017 Mheshimiwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisisitiza kuhusu uharaka na umuhimu wa kuwa na mahali pakuegeshea na kupandia na vituo vya daladala katika kituo cha Kimara, kwahiyo aliagiza TANROADS kutenga eneo kwaajili ya ujenzi wa mahali pakuegesha na kupandia Kimara Mwisho.