TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa za uzushi zinazoenezwa na watu wenye nia ovu kuhusu Mabasi mapya Yaendayo Haraka (Mwendokasi) kwamba, kuna Basi moja lilikuwa na hitilafu. Ukweli ni kwamba Mabasi yote 151 yaliyoingia nchini yapo katika hali nzuri na kwa sasa yamehifadhiwa katika Karakana ya Serikali iliyopo Mbagala Rangitatu yakisubiri maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza rasmi kutoa huduma kwa abiria.
Mnamo tarehe 30 Agosti 2025 basi moja lililokuwa na upungufu wa Gesi Asilia lililazimika kupaki pembeni ya barabara kwa dakika 10 ili kuongeza gesi na baada ya hapo lilielekea Karakana yalipo mabasi mengine.
Serikali itaendelea kutoa taarifa mbalimbali kuhusiana na usafiri wa umma Jijini Dar es Salaam.
Imetolewa na:
William V. Gatambi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)