Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
MAKATIBU WAKUU WAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA DART
27 Feb, 2026
MAKATIBU WAKUU WAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA DART

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na wenye Ulemavu Dkt. Jim James Yonazi ameongoza timu ya Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali za Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania kukagua maendeleo ya mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka –BRT pamoja na kukagua Mabasi mapya 100 yaliyoingizwa na kampuni ya UDART inayotoa huduma katika mradi wa DART Awamu ya Kwanza.

Akizungumza leo 27 Februari 2026  katika ziara hiyo, Dkt. Yonazi amesema kuwa lengo la Serikali ni kuendelea kuwapatia wakazi wa jiji la Dar es salaam usafiri bora, wa haraka na salama ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi sambamba na kurahisisha maisha kwa ujumla.

“ Tayari tunao watoa huduma watatu tunaye UDART, Mofat ambao tayari wanatoa huduma kwenye mradi wa DART awamu ya Kwanza na awamu ya Pili, pia ipo kampuni ya Emirates (Trans Dar)  ambayo Mabasi yake yapo njiani na yatakapo wasili yataingia kwenye kutoa huduma moja kwa moja .” Alisema Dkt. Yonazi

Vilevile Dkt. Yonasi amewataka UDART na watoa huduma wengine kuyatunza   mabasi yaliyopo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART Bw. Said Tunda ameeleza kuwa hivi karibuni wanatarajia kupokea mabasi mapya ya kampuni ya Emirates (Trans Dar).

Aidha Mtendaji Mkuu amefafanua kuwa pindi mabasi hayo yatakapokuja yanataraji kutoa huduma kwenye mradi wa DART Awamu ya Kwanza huku mtoa huduma wa hivi sasa  katika njia hiyo kampuni ya UDART atahamiakutoa katika mradi wa DART awamu ya Tatu inayoelekea Gongo la Mboto.

“Taasisi ya Tanroads ikikamilisha kujenga barabara watatukabidhi sisi DART ili tuweze kufunga miundombinu ya utozaji wa nauli. Na kikubwa kilichabakia ili kuanza kwa huduma gongo la mboto ni kukamilika kwa ujenzi wa karakana ambayo ndiyo roho ya BRT.”

Ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya mradi wa BRT ilijumuisha pia makatibu wakuu kutoka katika Wizara za Uchukuzi, Ujenzi, Fedha, Tamisemi, pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji mkuu wa Serikali.