Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
WAKALA WA DART WAENDELEA KUREJESHA HUDUMA ZA BRT BAADA YA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU SIKU YA TAREHE 29 OKTOBA 2025.
04 Nov, 2025
WAKALA WA DART WAENDELEA KUREJESHA HUDUMA ZA BRT BAADA YA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU SIKU YA TAREHE 29 OKTOBA 2025.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), unauarifu Umma kuwa unaendelea kuchukua hatua zote muhimu kurejesha huduma za Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) kufuatia matukio ya uharibifu yaliyotokea jijini Dar es Salaam tarehe 29 hadi 30 Oktoba, 2025.

Matukio hayo yalisababisha uharibifu mkubwa wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ikiwemo mabasi, vituo na vituo vikuu katika Barabara ya Morogoro (Awamu ya Kwanza) na Barabara ya Kilwa (Awamu ya Pili).

Wakala wa DART unasikitika kwa hali iliyotokea na unatoa pole kwa abiria wote walioathirika kutokana na usumbufu wa kusimama kwa huduma ya usafiri wa mabasi. Uharibifu huo unachelewesha jitihada za kuboresha usafiri wa umma kuwa  wa kisasa jijini Dar es Salaam.

Timu za kiufundi zipo kazini kufanya tathmini na matengenezo ya dharura ili kuhakikisha miundombinu muhimu inarejeshwa haraka. Lengo ni kuhakikisha huduma za BRT zinarejea mapema zikiwa salama na bora zaidi.

DART inawaomba wananchi kuwa na subra wakati huu ikifanya jitihada za kurejesha huduma. Kwa taarifa zaidi tafadhali endelea kutufuatilia kupitia tovuti yetu www.dart.go.tz  na kurasa zetu za mitandao ya kijamii @DARTMwendokasi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka - DART.