Rais Dkt. Samia Azindua Miundombinu na Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka awamu ya Pili, Awataka wananchi Kulinda Miundombinu.
Na. Mwandishi wetu DART.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan leo Agosti 7, ametembelea na kuzindua miundombinu ya Barabara za mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa, Chang’ombe Sokoine na Kawawa na Kuwata wananchi kuilinda miundombinu hiyo kwani inajengwa kwa thamani kubwa.
Akizungumza katika viwanja vya ufunguzi eneo la Kwa Azizi Temeke Jijini Dar es Salaam, Mh Rais amesema kila mwananchi ni lazima awe mlinzi namba moja wa mioundombinu ambayo Serikali inaijenga kwa fedha nyingi za Wafadhili na za Walipa kodi ambayo lengo lake niwapunguzia adha ya usafiri wakazi wa Jiji la Dar es Salam na maeneo ya Jirani.
“Mtu yeyote atakayekutwa anahujumu miundombinu hii nilazima tumchukulie kama mhujumu Uchumi ili miundombinu hii iweze kudumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya kizazi hiki na manufaa ya kizazi kijacho” Alisema Mh. Rais.
Aidha Mh.Rais, ameelekeza Wakala wa Mabasi Yaendayo Haaka DART kuharakisha upatikanaji wa mtoa huduma ya Mabasi katika Awamu ya Tatu ya Mradi unaoelekea Gongolamboto kwakuzingatia mahitaji.
“Niwatake Wasimamizi wa Mradi Huu wenzetu wa DART kuhakikisha wanatafuta kwa haraka mtoa hduma ya Mabasi kule wenye awamu ya Tatu Gongolamboto kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo hayo” Alisema Dkt.Samia.
Mh.Dkt Samia alisema kuanza kwa utekelezai wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili sio tu kumewapunguzia adha ya usafiri wakazi wa Mbagala na maeneo ya Jirani bali kumeongeza ajira kwa vijana jambo mbalo limeelekezwa katikaIlani ya Chama cha Mapinduzi.
“Nimeona vijana wengi wanafanya kazi za kukatisha tiketi katika Vituo vya Mwendokasi hii ndio tathmini halisi ya maendeleo kwani uwepo wa mradi huu umewawezesha kupata ajira na hatimaye kujipatia kipato” Alisema Dkt.Samia.
Kwa upande wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr. Sid Ould Tah amesema Benki yake itaendelea kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo ambayo inaleta suluhisho la matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi kama ilivyo kwa mradi wa BRT Awamu ya Pili.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Prof Riziki Shemdoe katika salamu zake alimweleza Mh.Rais kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira watahakikisha wanatumia fursa ya matumizi ya Gesi kwenye Mabasi kama chanzo cha mapato.
“Mh.Rais kwauwa Mabasi haya yanatumia nisati safi mimi nitakaa na wenzangu na tutaangalia namna ya kupata fedha kwani tunapunguza sana hewa ya ukaa ambayo ingezalishwa kama Mabasi haya yasingetumia nishati hii ya gesi” Alisema Waziri Shemdoe.
Katika hatua Nyingine Waziri wa Ujenzi Mh.Abdalah Ulega alimuomba Rais Dkt. Samia barabara zinazoishia Mbagala Rangi Tatu, Gongolamboto na Boko kweye awamu za Pili za Tatu na Nne za mradi wa BRT ziongezwe hadi kufikia maeneo ya Vikindu,Kisarawe,Bagamoyo na Kibaha ili miundombinu hiyo iweze kuunganisha Mkoa wa Dar es Salaaam na Pwani jambo ambalo Mh Rais alilikubali.
Mwisho.
