KUSITISHA VIBALI VYOTE VYA KUPITA KWENYE BARABARA ZA BRT
KUSITISHA VIBALI VYOTE VYA KUPITA KWENYE BARABARA ZA BRT
10 Dec, 2025
Pakua
TAARIFA KWA UMMA
YAH: KUSITISHA VIBALI VYOTE VYA KUPITA KWENYE BARABARA ZA BRT
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), unautaarifu umma kuwa kuanzia sasa, vyombo vyote vya usafiri isipokuwa Mabasi Yaendayo Haraka haviruhusiwi kutumia njia maalum za Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).
DART inasisitiza kuwa vibali vyote vilivyowahi kutolewa vimesitishwa kuanzia tarehe tajwa. Doria na udhibiti vitaimarishwa ili kuhakikisha agizo hili linazingatiwa. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
Aidha, DART inatoa wito kwa wananchi wote kushirikiana kulinda miundombinu ya BRT.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART
10 Desemba 2025
