Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

"Usafiri wa Umma Nadhifu"

DART Logo
Rose Kagali
Rose Kagali

Mtoa huduma kitendo cha Huduma kwa watu wenye Mahitaji Maalum(Social)

Anasema,‘‘Tunafanya kazi kama timu tukishirikiana,ikitokea abiria kapata changamoto ya ugonjwa huwa tunamsaidia kumpa huduma ya kwanza,hata tukimpeleka hospitali iliyopo karibu huwa wanatupatia ushirikiano kuhakikisha mgonjwa anakuwa salama,kuna kipindi huwa tunatoa pesa zetu mfukoni,ikiwa mgonjwa hana uwezo au ndugu wa kumsaidia kwa wakati huo.’’

Kwa upande wa huduma maalum kwa Mabasi ya wanafunzi Rose anasema ,‘‘ Kwa asubuhi na jioni huwa kunakuwa na mabasi mawili kwa ajili ya wanafunzi tu,na kila gari tunakuwa na mhudumu wa kitengo chetu kwa ajili ya kusindikiza gari kuhakikisha wanafunzi wanasafiri salama mpaka mwisho wa basi.’’